|
NJIA RAHISI YA WOKOVU WA MUNGURafiki yangu:Ninakuuliza swali muhimu maishani mwako. Furaha yako ya milele au huzuni yako ya milele inategemea jibu Ia swali hili. Swali ni hili:Je, umeokolewa?Si swali la jinsi ulivyo mwema, wala si swali la kama u mshiriki wa kanisa, bali:Je, umeokolewa? Una uhakika kwamba utaenda mbinguni utakapokufa? Mungu anasema kwamba, ili uende mbinguni, ni lazima uzaliwe mara ya pili. Katika Yohana 3:7, Yesu alisema kwa Nikodemo, “Ni lazima uzaliwe mara ya pili.” Katika Biblia Mungu anatupatia njia ya pekee ya kuzaliwa mara ya pili, yaani kuokolewa.Njia yake ni rahisi! Unaweza kuokolewa leo. Vipi? Kwanza, rafiki yangu, ni lazima utambue kwambawewe u mwenye dhambi.“Kwa sababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”(Warumi 3:23). Kwa sababu u mwenye dhambi,umehukumiwa kufa.“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti”(Warumi 6:23). Hii ina maana kutengwa na Mungu katika jehanum milele.“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”(Waebrania 9:27). Lakini Mungu alikupenda mno hata akamtoa Mwanawe pekee, Yesu, ili azichukue dhambi zako na kufa pahali pako.“Yeye asiyejua dhambi[Yesu, ambaye hakujua dhambi yo yote]alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye”(2 Wakorintho 5:21). Ilimbidi Yesu amwage damu yake na kufa.“Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu”(Mambo ya Walawi 17:11).“. . . Pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo[msamaha]”(Waebrania 9:22). “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi”(Warumi 5:8). Ingawa hatuelewi ni jinsi gani, Mungu alisema kuwa dhambi zangu na dhambi zako ziliwekwa juu ya Yesu naalikufa pahali petu.Yesu akawafidia yetu[badala yetu].Ni kweli. Mungu hawezi kusema uongo. Rafiki yangu,“Mungu . . . anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu”(Matendo 17:30). Kutubu huku au toba hii ni badiliko la nia akilini; kukubaliana na Mungu kuwa mtu ni mwenye dhambi, na kukubaliana na yale aliyoyafanya Yesu kwa ajili yetu msalabani. Katika Matendo 16:30-31, mlinzi wa gereza wa Filipi aliwauliza Paulo na Sila,“Mabwana, yanipasa nifanye nini nipatekuokoka?Wakamwambia,mwaminiBwana Yesu, nawe utaokoka . . . .” Mwamini tu Bwana Yesu ambaye alibeba dhambi zako, akafa badala yako, akazikwa, na Mungu alimfufua.Ufufuo wake unahakikisha kwa nguvukuwa aaminiye anaweza kudai uzima wa milele anapompokea Yesu kuwa Mwokozi wake. “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”(Yohana 1:12). “Kwa kuwakilaatakayeliitia jina la Bwanaataokoka”(Warumi 10:13). Neno“kila”linakujumlisha na wewe.“Ataokoka,” maana yake si labda, au inawezekana, bali ni kwa uhakika“ataokoka.” Hakika, unatambua kuwa u mwenye dhambi? Po pote ulipo sasa hivi, ukitubu, inua moyo wako kwa Mungu katika maombi. Katika Luka 18:13, mwenye dhambi mmoja aliomba:“Ee Mungu, uniwie radhimimi mwenye dhambi.”Basi omba:“Ee Mungu, ninajua kuwa ni mwenye dhambi. Ninaamini kuwa Yesu alikuwa fidia yangu alipokufa msalabani. Ninaamini damu yake aliyomwaga, kufa kwake, kuzikwa kwake, na kufufuka kwake kulikuwa kwa ajili yangu. Sasa ninampokea awe Mwokozi wangu. Asante kwa msamaha wa dhambi zangu, zawadi ya wokovu na uzima wa milele, kwa sababu ya neema yako ya huruma. Amina.” Mwamini Mungu katika Neno lake, na dai wokovu wake kwa imani. Amini, na utaokoka. Hakuna kanisa, wala jumba, wala matendo mema yawezayo kukuokoa.Kumbuka, Mungu ndiye aokoaye. Basi!
Njia rahisi ya wokovu ya Mungu ni:Wewe u mwenye dhambi na usipomwamini Yesu ambaye alikufa pahali pako, utakaa milele jehanum. Ukimwamini kuwa Mwokozi wako ambaye alisulubiwa, akazikwa, akafufuka, utapokea msamaha wa dhambi zako zote, na utapokea zawadi [karama] ya uzima wa milele kwa imani. Unasema, “Kweli, haiwezi kuwa rahisi hivi.”Ndiyo, ni rahisi hivyo! Ndivyo ulivyo mpango wa Mungu wa wokovu katika Maandiko.Rafiki yangu, mwamini Yesu na kumpokea kuwa Mwokozi wako leo. Ikiwa huu mpango wake wa wokovu hauko wazi au haueleweki kwako, soma kijikaratasi hiki tena na tena, pasipo kukiweka chini, mpaka umeuelewa ujumbe wake. Nafsi yako ni ya thamani zaidi kuliko vyote vya ulimwengu. “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?”(Marko 8:36). Hakikisha kwamba umeokoka. Ukipoteza nafsi yako utapoteza mbingu na utapoteza vyote. Tafadhali, mruhusu Mungu akuokoe sasa hivi. Nguvu ya Mungu itakuokoa, itakulinda, na kukuwezesha kuishi maisha ya ushindi ya Kikristo.“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”(1 Wakorintho 10:13). Usitegemee hisia zako – jinsi unavyojisikia. Hisia zinabadilika-badilika. Simama juu ya ahadi za Mungu. Ahadi za Mungu hazibadiliki. Ukiisha kuokoka, kuna mambo matatu ya kufanya kila siku ili ukue kiroho:Omba– unazungumza na Mungu.Soma Biblia yako– Mungu anazungumza nawe.Shuhudia– waambie watu wengine kwa niaba ya Mungu. Unapaswa kubatizwa katika utii kwa Bwana Yesu Kristo kuwa ushuhuda wa hadhara wa wokovu wako, halafu, bila kuchelewa, jiunge na kanisa ambalo linaamini Biblia.“Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu . . . ”(2 Timotheo 1:8). “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni”(Mathayo 10:32). Ford Porter, Mwandishi |